UJENZI SOKO LA MWANAKWEREKWE UMEFIKIA ASILIMIA 98

Kiasi cha wafanyabiasha elfu tatu mia mbili ishirini na mbili, waliopisha ujenzi wa soko jipya la Mwanakwerekwe, watapewa kipaumbele kuhamia katika soko hilo.
Mkuu wa Soko la Mwanakwerekwe C, Sharif Ali Sharif, amesema hatua inayoendelea kwa sasa ni kufanya uhakiki wa majina ya wafanyabiashara hao ili kujiridhisha.
Amesema mbali na hao, zaidi ya maombi mia mbili ya wafanyabiashara wengine wanaotaka nafasi za biashara yamepokelewa, ambapo soko hilo lina uwezo wa kuchukua zaidi ya wafanyabiasharà elfu tano.
Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Magharib 'B', Khadija Said amesema ujenzi wa soko la Mwanakwerekwe, umezingatia wafanyabiashara wa aina zote, na kuwataka kuhakikisha soko linabaki katika hali ya usafi na kulitunza ili lidumu kwa muda mrefu.
Mkandarasi wa ujenzi huo, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Uchumi JKU, Kanal Makame Abdullah Daima, amesema ujenzi huo umeshafikia asilimia 98, hadi sasa na unatarajia kukamilika mwisho wa mwezi wa 5 mwaka huu.
Nao baadhi ya wafanyabiashara wameomba kuwekwa mazingira mazuri yatakayowawezesha kufanya biashara zao bila usumbufu.

Пікірлер: 3

  • @jakobongwara3038
    @jakobongwara3038Ай бұрын

    Hongela saana viongozi kwakutenda haki

  • @musaakim2853
    @musaakim2853Ай бұрын

    Tayari mshawatengezea ullaji wengine wengine ambao huitwa [manucipal] nalitakua chavu kama choo sio muda mrefu na watanganyika mamanitilie

  • @user-hk2oz2eg4j
    @user-hk2oz2eg4j2 ай бұрын

    Manispaa wanashindwa kutekeleza usafi kwenye masoko. Wakati wafanya biashara wanalipa kodi ikiwemo na suala la usafi.

Келесі