UZINDUZI WA MAGARI YA KUBEBEA TAKA MANISPAA YA MAGHARIBI 'A'

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ, Mh Masoud Ali Mohammed, amesema kukabidhiwa magari ya taka iwe ni kuleta mageuzi ambayo yatachangia kuweka miji katika mazingira mazuri.
Akizundua magari ya usafi kwa Baraza la Manispaa Magharib A na kukabidhi vyeti kwa Makampuni yaliyosaidia katika zoezi zima la uzowaji na ubebaji taka, amesema suala la usafi linamuhusu kila mmoja kwa nafasi yake, na kuwataka masheha kuwachukulia hatua watu wanaovunja sheria ya kutupa taka ovyo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Magharib A Mbaraka Said Hasuni amesema Watayatumia magari hayo kwa umakini ili kuhakikisha yanatumiwa kwa muda mrefu kwa malengo yaliyokusudia.
Meneja wa Amana bank, Suleiman Suleiman ,amesema wataendelea kuhamasisha utumiaji wa benki ya amana, kwani wanawawezesha wafanyabiashara wakubwa na wadogo kuinua vipato vyao na kukuza pato la Nchi.
Nae Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, wilaya ya mfenesini, Keis Mashaka Ngusa, amesema kuimarisha Afya za Wananchi ni miongoni mwa utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi kuhakikisha kuwa jamii inapambana na mazingira ya uchafu.
Jumla ya Magari matano yaliyokabidhiwa yamegharim shilingi milioni Mia nane na thalathini.

Пікірлер