Profesa Issa Shivji: Tusikubali Kuwa Nchi ya Kufanyiwa Majaribio, Ni Juu ya Dira ya Taifa 2050

Profesa Shivji: Dira ya Taifa Haina Muda Maalum.Tusikubali Kufanyiwa Majaribio
Akizungumza leo Juni 08,2024, katika kongamano la kwanza la kitaifa la maandalizi ya dira ya taifa ya maendeleo lililofanyika katika ukumbi wa Nkurumah, Profesa Issa Shivji ameeleza kuwa dira ya taifa ni tofauti na mipango ya maendeleo yenye muda maalum.
"Dira haina maana ya mpango wa maendeleo, mpango wa maendeleo unakuwa wa muda maalum. Kwa maoni yangu dira haina muda maalum," ameeleza Profesa Shivji.
Profesa Shivji alifafanua Zaidi kuwa moja ya mfano wa dira ya taifa ni Azimio la Arusha. Akijibu hoja hii Waziri wa OR Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo alieleza kuwa wameyapokea maoni hayo.
Katika wasilisho lake hilo Shivji ameasa juu ya taifa kuepuka kufanyiwa majaribio katika utengenezaji wa dira yake.
"Tusikubali kufanyiwa majaribio, majaribio yaliyofanyika miaka ya 1960 yanatosha. Tuwashirikishe wananchi kikamilifu popote pale walipo tupate maoni yao kuhusu nchi wanayotaka, Tanzania wanayoitamani, matamanio yao yapewe kipaumbele.Hii haiwezekani bila kuwa na mjadala wa kitaifa," alieleza Profesa Shivji.
Alifafanua Zaidi: "Tusifanye ile tuliyozoea wananchi wanatoa maoni, halafu wataalamu ndio wanachambua maoni haya. Popote pale walipo wananchi; vijijini, viwandani, mashuleni na kadhalika ili kujenga muafaka wa nchi tunayoitaka. Na mengine ya kupanga mpango wa muda mrefu wa muda mfupi itafuata."

Пікірлер: 16

  • @joycebayo8106
    @joycebayo810628 күн бұрын

    Nimekubali lecturing ya professor Issa shivji, you will be my teacher forever. Your professionalism will remain in the heart of Tanzanian forever.

  • @stephenndagalla8183
    @stephenndagalla818328 күн бұрын

    Maoni mazuri ya Prof Shivji. Wkt wanachi wakishirikishwa kikamilifu kutoa maoni ya DIRA ya Taifa, Serikali kwanza iwaelimishe wananchi aina na kiasi pia matumizi ya Raslimali zote muhimu zilizomo Nchini.

  • @edwardgafachu8932
    @edwardgafachu893229 күн бұрын

    Kweli kabisa tufanye mijadala kama hii mingi kabla ya kuwapa wataalamu kututengenezea mipango ya kinadharia isiyotekelezeka. Asante profesa.

  • @user-pf2qk8fz9o
    @user-pf2qk8fz9o28 күн бұрын

    Asante sana mzee professor kwa darasa huru yaaani unaongelea mambo kwa kuunganisha dot kama slow poison 😊😊

  • @omarilugendo8663
    @omarilugendo866328 күн бұрын

    Tunachangamoto kubwa ya wanasayansi katika kila nyanja muhimu nadhani ingefanyika tathmini kwanza ya uwezo wa kuandaa DIRA kisayansi ili tusije kuingia kwenye mtego ule ule wa Miaka 60 iliyopota. Given mazingira ya Dunia inahitaji zaidi ya Ujanja (smartness) kuweza kukwepa mitego ya Mataifa makubwa Duniani ambayo yanafaidika na hali tuliyonayo. Safari ni ngumu na ndefu lakini hatuna budi kuianza. Mungu ibariki Afrika , Mungu ibariki Tanzania.

  • @thomaskwibonelwa9240
    @thomaskwibonelwa924028 күн бұрын

    Hawa ndo think-tank wanaotakiwa. Na siyo chawa- watengeneza dira.

  • @juliuskitaluka1206
    @juliuskitaluka120629 күн бұрын

    Akili kubwa

  • @zobakazizi7637
    @zobakazizi763728 күн бұрын

    Serikali imeshindwa kusimamia kampuni za Kitanzania kuendesha BRT. Anapewa mwarabu. Atakusanya fedha atazipeleka kwao. Ataondoa fedha nchi na kuzipeleka nje.

  • @joycebayo8106
    @joycebayo810628 күн бұрын

    Hakika kama watanzania hatujutii wew kusomeshwa na rasilimali ya wazazi wako na ya Tanzania, wew ni mtanzania mkweli.

  • @MasoudyMichael-ox7xl
    @MasoudyMichael-ox7xl28 күн бұрын

    Mzee saivi watu Ni machawa tu😅

  • @Sr.BasilisaPanga
    @Sr.BasilisaPanga28 күн бұрын

    Je,vijana. Wananchi, wattaalam,hasa wanauchumi, wanasheria wanao uwezo wa kuona mbele, wanao uzalendo, wako huru, tunaelewa mambo muhimu kwenye Dirac? Na je, wale wananchi wachache waliozoea kupanga Dirac ya taufa kwa maslahi yao wamelala?

  • @oscarsagara8813

    @oscarsagara8813

    28 күн бұрын

    Na aidha hata hawaelewi kabisa kilichosemwa na proff hapa...,amewachanganya kabisa.

  • @evelynmwaimu-vd9jo
    @evelynmwaimu-vd9jo27 күн бұрын

    Kwani hawa wanathaminiwa??? Kulliko wasaniiii!!!

  • @ProsperMwakasungura
    @ProsperMwakasungura28 күн бұрын

    Sasa wewe jifanye huelewi kana kwamba wenye dhamana hawaelewi.

Келесі