Tazama Biteko alivyombananisha Mkurugenzi wa Tanesco Tabora, atoa siku 7...

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Tanzania, Dk Doto Biteko Julai 7, alikuwa Sikonge mkoani Tabora kukagua mradi wa umeme wa Kilovoti 132 ambapo akiwa kwenye kituo hicho akawabana watumishi wa Tanesco, akiwemo mkurugenzi wa shirika hilo hapa nchini kuhusiana na kusuasua kuanza utekelezaji wa vituo vya kupooza umeme katika maeneo mbalimbali nchini.
Hata hivyo, Dk Biteko ameonekana kukerwa na mmoja wa watumishi wa shirika hilo aliyeoonekana kumdanganya kwenye maelezo yake, jambo lililozua sintofahamu kwenye mkutano na wananchi.
Baada ya hilo kutokea akatoa siku saba kwa Tanesco wawe wameleta mpango wa kujenga vituo vya kupooza umeme nje ya Dar es salaam tofauti na hali ilivyo sasa.

Пікірлер: 3

  • @YusufSasamalo-uz4ii
    @YusufSasamalo-uz4ii13 күн бұрын

    Wataalam Wataalam wetu is the problem

  • @fidelfidel-jz4iw
    @fidelfidel-jz4iw13 күн бұрын

    Wataamu wetu huwa wanajitoa akili hebu fikilia eti center ipo Dar sasa huoni kuna shida hapo hata mamuma ataelewa tu hao tanesco shida sana wanajulikana mambo yao

  • @Anti-socialSocialClub
    @Anti-socialSocialClub13 күн бұрын

    Tatizo ni kwamba wanafanya kazi wa umma wote wanakimbilia vikao na safari badala ya kufanya kazi zao. Kuna posho nyingi mno kwenye safari na vikao...punguzeni posho !

Келесі