JE, UNAFAHAMU TATIZO LA MGUU KIFUNDO AU NYAYO ZILIZOPINDA?

NA ALBERT G. SENGO/MWANZA
Mguu kifundo ni aina ya ulemavu ambao mtoto anazaliwa nao baada ya kupatikana na hitilafu katika mifupa ya kwenye nyayo. Chanzo cha tatizo hilo hakijakuwa bayana ila wahusika hulazimika kutembea kwa kutumia sehemu ya nje ya unyayo, hali inayoleta matatizo na shaka katika ufanisi.
MDH inashirikiana na Serikali kwa ufadhili wa Miracle Feet katika utoaji wa huduma za Mguu kifundo na matibabu yake na hii ndiyo kazi inayofanyika Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza, ambapo Kipindi cha DRIVE MIX kutoka radio Jembe Fm kinazungumza na Dr. Mussa Hamisi kujua undani wa changamoto hiyo.

Пікірлер