UGOMVI WA FAMILIA KUKOSA MALEZI YA KIROHO MATUNZO AFYA YA MWILI SABABU ZA ONGEZEKO LA WATOTO MITAANI

NA ALBERT G. SENGO/MWANZA
Ni jambo lililowazi kwamba hakuna jamii hasa ile inayojielewa, inayoweza kufurahia kuona watoto wakitenganishwa na familia zao.
Ugomvi wa baba na mama, malezi ya mzazi mmoja yanayopelekea kushindwa kumudu mahitaji, kukosa malezi ya kiroho, elimu, matunzo ya afya ya mwili ni moja kati ya sababu alizozitoa Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe. Angeline mabula zinazochangia ongezeko la watoto wa mitaani.
Mabula ameyasema hao katika hafla maalum ya maadhimisho ya siku ya mama duniani iliyofanyika mwishoni mwa juma, siku hiyo ikiambatana na kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwake ambapo mbunge huyo aliamua kuitumia kwa kutoa misaaada kwa kituo cha watoto wenye uhitaji cha Fonerisco kilichopo wilayani Ilemela mkoani Mwanza.
#samiasuluhuhassan
#mwanza
#ILEMELA
#Angelina_Mabula

Пікірлер

    Келесі