Fahamu siri ya mlango mkongwe zaidi Zanzibar

Moja ya miji ya kihistoria inayotambuliwa na Shirika la Umoja wa mataifa la UNESCO kama urithi wa dunia, ni Mji Mkongwe, ama Stone Town, ZANZIBAR.
Moja ya sifa kubwa ya mji huu ni upekee wa Milango ya nyumba zake inayoupa umaarufu mkubwa na kuvutia wageni.
Milango hii ni mikongwe na inayoweza kudumu kwa zaidi ya miaka 200, inaitwa Milango ya Zanzibar ama Zanzibar Door.
Mwandishi wetu Yusuph Mazimu ametembelea mji huo na kukuta mlango unaotajwa kuwa mkongwe zaidi Zanzibar na moja ya milango mikongwe zaidi Afrika. Una miaka zaidi ya 400. Je nini siri ya kudumu kwa milango ya Zanzibar?
#bbcswahili #bbcswahili65 #zanzibar

Пікірлер: 1

  • @hajiabdalla5772
    @hajiabdalla5772 Жыл бұрын

    Wa marehemu beilt ajaib wa mwanzo ila CCM washauuza na mwengine upo joz kona