Ukaguzi magari ya wanafunzi Mwanza, RPC Mutafungwa aonya

Wakati shule za msingi na sekondari nchini zikitarajiwa kufunguliwa Juni mosi, 2024 Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limezindua kampeni ya wiki ya ukaguzi wa magari yanayotoa huduma za usafirishaji wa wanafunzi katika shule za umma na binafsi jijini humo.
Kampeni hiyo imezinduliwa leo Jumatatu Juni 24, 2024 na Kamanda wa Polisi (RPC) Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa, huku magari zaidi ya 55 yakianza kufanyiwa ukaguzi huo kabla ya kuruhusiwa kuanza kutoa huduma pindi shule zitakapofunguliwa.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani (RTO) mkoani humo, Sunday Ibrahim amesema tayari magari zaidi ya 50 yamefikishwa katika gereji hiyo kwa ajili ya ukaguzi, huku akiahidi kutoa taarifa ya matokeo ya kampeni hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya wamiliki wa shule, Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Shule binafsi Ilemela mkoani humo, Ezekiel Molel amewataka wenye magari yanayotoa huduma hiyo kutokacha ukaguzi huo, huku akiahidi ‘kuwachoma’ watakaokacha ukaguzi huo.

Пікірлер

    Келесі