TANROADS GEITA YAKAMILISHA USANIFU BARABARA YA USHIROMBO-NYIKONGA-KATORO

Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) imetekeleza maelekezo ya Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa kwa kukamilisha Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina wa Barabara ya Ushirombo - Nyikonga - Katoro (58km). Kipande cha Nikonga - Kashelo (10.48km) pamoja na Daraja la Nyikonga, kipande cha Kashelo - Ilolangulu (15.0km) na kipande cha Ushirombo (Kilimahewa) - Nanda (15.57km) vyenye jumla ya km 41.05 vipo kwenye hatua ya kumtafuta Mkandarasi wa kuanza Ujenzi kwa kiwango cha Lami.
Vile Vile Serikali ipo katika maadalizi ya kutangaza kipande cha barabara ya Ushirombo - Kashelo (22.5km) ili kumpata Mkandarasi wa kuanza Ujenzi kwa kiwango cha LamiWaziri Bashungwa alitoa maelekezo hayo kwa TANROADS tarehe 08 Juni, 2024 katika mkutano wa hadhara wa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Bukombe, Dkt. Dotto Biteko katika Kata ya Katome Mkoani Geita.
Akizungumza mara baada ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali, Kaimu Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Geita Mhandisi Fredrick Mande amesema kuwa Katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan miradi mbalimbali ya maendeleo imetekelezwa ikiwa ni Pamoja na miradi ya matengenezo.

Пікірлер