Salama Na Fid Q Ep 7 | NGOSHA WA MBASA Part 2

#YAHStoneTown #SalamaNa #PodCast
Listen our Podcast on
‪Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcasts Link apple.co/2Ou1bru‬
‪KZread Link bit.ly/KZreadSalamaNa
NGOSHA WA MBASA
Nakumbuka kipindi ambacho Fidi alikua anaamini kabisa kama kuweka ‘uso wa mbuzi’ ndo kulikua kunakufanya uwe ‘hard core’, sina uhakika lini aliachana na dhana hiyo ila kwa kipindi cha miaka miwili au zaidi tabasamu na bashasha vimekua havibanduki kwenye uso wake, jambo ambalo mimi kama rafiki nalifurahia sana. Nakumbuka baadhi ya marafiki zangu wa kike ambao ni wapenzi haswa wa mziki wake walikua wakiniambia eh, sema rafiki yako mgumu jamani, Kha! Mi hucheka tu na baadae wakishazoeana basi sidhani kama kuna hata mmoja anaweza kusema kitu kibaya kuhusu yeye. Nilikua nacheka kwasababu mimi naamini namfahamu rafiki yangu huyu, yeye hupenda sana matani, na kucheka na marafiki wa karibu wanaweza wakathibitisha hilo maana katika watu ambao unaweza ukawatania weeee mpaka asubuhi, na utani mpaka wa vitu vyengine ambavyo wewe wa karibu unaweza kusema ey, hiyo sasa imepitiliza, yeye waala... Atacheka tu!
Mwenye kipaji chake cha kujifunza mwenyewe, nasema hivyo kwasababu nadhani kufahamiana kwetu na kuelewana kwetu pia kunatokana na kuwa na vitu vinavyofanana ndani yetu. Kajifunza jinsi ya kupenda kusoma vitabu mwenyewe, kujifunza jinsi ya kuandika na kurap mwenyewe, kajiendeleza mwenyewe (bila ya shaka kuna watu walomsaidia kwa tafu za hapa na pale ila walitokea baada ya kuona jitihada zake). Alihakikisha anasafiri kwenda nje ya nchi na Africa kwa jitihada zake mwenyewe na mpaka leo, kukiitwa watu ambao wamesaidia kwa kiasi kikubwa kufikisha Hip Hop ya nyumbani hapa ilipo basi jina lake litakua ni miungoni ya yale yatakayopata heshima ya juu kabisa. Pia anachekesha sana. Uelewa wake wa baadhi ya vitu unaweza ukakuacha mdomo wazi wakati mwengine. Kwenye uwepo wake? Vicheko lazima vitawale.
Hii siku nilitia nae story haikua kama kazi, bali kama mtu na rafikiye tu wakitia story juu ya njia za maisha ambazo tumepitia mpaka sasa. Fidi amekuzwa na Mama yake ambae alikua ni mfanyakazi wa serikalini (ameshastaafu), alikulia mkoani kama wengi wetu, alifika Dar akakaa kwa ndugu kama wengi wetu, alianzia sehemu na kutoka hapo mdogomdogo akajijenga kufikia hapa alipo. Humu tumeongelea hayo, watoto, muziki, ndoa, maisha ya wasanii na maendeleo kwa ujumla. Yangu matumaini uta enjoy na kuelewa baadhi ya vitu zaidi na zaidi.
Here’s to Ngosha wa Mbasa.
Love,
Salama.
Follow:
Twitter: / yahstonetown
Instagram: / yahstonetown
Facebook: / yahstonetown

Пікірлер: 142

  • @latriciah01augustino67
    @latriciah01augustino674 жыл бұрын

    Mafanikio ni nini? Jitengenezee tafsiri yako kisha ishi nayo🙌🏽🙌🏽🙌🏽 Ahsante fid

  • @christopherjames3684
    @christopherjames36844 жыл бұрын

    Hii ni zaidi ya shule asente salama kwa kutuletea mtu kama hyu anaetujenga kwa maongezi herimu nzuri sana hii...

  • @abdulaziz703
    @abdulaziz7034 жыл бұрын

    Ngosha, we jamaa nakukubali always. Umenifanya niipe kazi akili yangu kuchanganua maana ya maneno kwenye mistari ya nyimbo zako. Binafsi sijutii kufahamu pamoja na kusikiliza chochote kinachotoka kinywani mwako coz naamini utakuwa hujakitoa kwa bahati mbaya.

  • @joycekinyange6179
    @joycekinyange6179 Жыл бұрын

    Yaani Fid Q is so deep, appreciate you sharing your story and experiences especially around single parenthood and blended family life. You are doing a great job and an exemplary role model for others in similar circumstances. Asante bro, continue living your truth 🙏🏽

  • @ffredy70
    @ffredy704 жыл бұрын

    Best interview ever

  • @abbysauko3725
    @abbysauko37254 жыл бұрын

    Yan muuliza maswal ametulia kwenye kuuliza na anaejibu maswal ametulia kwenye kujibu..

  • @paulolwila4253
    @paulolwila42534 жыл бұрын

    Nampenda Bure salama namna alivyopoz sio wanahabr wengine huwez jua nan ana muitaview muingine coz wote unakuta waongeaz mpka c poah but hapa salama karelax fid Q anaflow vzr sana. Love you all .

  • @deustrackson6035
    @deustrackson60353 жыл бұрын

    Unaeza mckiliza fid badae ukahisi ulisoma ktabu Cha professor flan.......MAY GOD BLESS U MUCH BRO

  • @simonsanga2129
    @simonsanga21294 жыл бұрын

    Salama big up,can you bring his friend Nikki wa Pili

  • @kapagaanimalcare5523
    @kapagaanimalcare55234 жыл бұрын

    Naenjoy na kujifunza kwenye kila interview ninayo kusikiliz na uwa siachi interview yoyote inipite ambayo umeojiwa. WE NI DARASA LINALOTEMBEA, MZIKI WAKO NI SHULE TOSHA

  • @abdallahmakombo3866
    @abdallahmakombo38664 жыл бұрын

    Hiki kichwa hiki ,kweli maisha NI elimu na SI ya darasani NI vitabu tu,Kisha uhalisia !!,

  • @kingungeii6520
    @kingungeii65204 жыл бұрын

    Fid Q ni chanzo cha busara yangu

  • @peninaancon1256
    @peninaancon12564 жыл бұрын

    Exactly, Mafanikio ni kujitengenezea tafsiri yako na kuiishi kila siku..

  • @erickmbiso9939
    @erickmbiso99394 жыл бұрын

    Interview iko vzr san jinsi unauliza maswali na anavyojibu iko poa sana nadhan ndio salama na best mpaka sasa lakini jaribu kumpa airtime Niki mbishi amwage madini yake

  • @philimonsoka2325
    @philimonsoka23254 жыл бұрын

    The best hip hop artist ever in tanzania

  • @bonniegtmagabe2009
    @bonniegtmagabe20094 жыл бұрын

    kama kuna kitu mmegundua kweny hii interview...sio intervention ya mwaka huu niya mwaka jana....kwhyo ilkuw imefanywa tayar...🔥🔥🔥

  • @elninothetragedy3121
    @elninothetragedy31214 жыл бұрын

    Fid nakuelewa sana... nakumbuka KAN Festival nlivamia jukwaa ulivyopanda tu... duh nakukubali sana bro

  • @ahmedaziz7853
    @ahmedaziz78534 жыл бұрын

    Nimetaman sana hii interview isiishe madini ya ghali sana yapo humu

  • @johnpantaleo6962
    @johnpantaleo69624 жыл бұрын

    Dah nimepata faida kubwa sana kuingalia hii interview kwani nimejifunza kitu kikubwa sana kutoka kwa fid q

  • @adamidrisa9232
    @adamidrisa92324 жыл бұрын

    sema salama ni kizuri kinyama big up sn kwahuyo muhuni anae ishi na huyu manzi