Salama Na ANNA TIBAIJUKA SE6 EP58 | LA PROFESSEUR PART 1 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460

Ойын-сауық

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
Nilipoandikiwa ujumbe mfupi na Edwin Bruno ambaye ni mkwe wa Professor kwamba Mama amekubalia kufanya kipindi na sisi siku hiyo ya Jumapili akishatoka church nilihisi kama naota. Mwenyezi Mungu anajua kwa kiasi gani tumekua tukitaka kufanya maongezi nae kwenye kipindi chetu. U busy wake na pengine mara nyingi kutokuwepo Dar es Salaam napo palikua panaleta ugumu, nyengine ilkua ni tarehe zetu za kufanya production na availability yake zilikua zinapishana sana. So unaweza ukaelewa excitement ambayo nilikua nayo baada ya finally samaki kujaa kwenye ndoana.
Professor Anna Tibaijuka ni LEGEND miongoni ma magwiji kwenye nchi hii kwa kazi yake na usomi wake na uzazi wake na kujibeba kwake. Kazi mbali mbali ambazo amewahi kuzifanya na kuliwakilisha Taifa hili zinajizungumza kwa sauti kubwa. Ila Safari yake mpaka anafikia kwenda kufanya kazi kwenye Taasisi kubwa duniani hakukumdondokea tu miguuni. Usomi wake ambao aliupambania toka akiwa mdogo na kupata ushirikiano kutoka kwa Marehemu Baba yake ndo kila kitu. Enzi ambazo mtoto wa kike alikua anaandaliwa kuwa Mama wa nyumbani, Baba yake aliamini zaidi kwenye kumpeleka mtoto wake shuleni na kwa mujibu wa Mama Tibaijuka Baba yake alikua aliwasisitiza wazee wenzake kufanya hivyo maana dunia ndo ilikua inaelekea huko, kuna ambao walimsikiliza na wengine ambao waliona anapoteza tu pesa na muda.
Mama Tibaijuka na Mimi tuliongelea kuhusu gharama za elimu enzi hizo Mimi nikidhani elimu “ilikua bure” pasi na kujua elimu kipindi hiko ilikua ghali pengine kuliko sasa na ukichukulia shule zenyewe zilikua mbali kweli kweli. Ananiambia pia suala la yeye kutaka kutomuangusha Baba yake ambaye baadhi ya watu walikua wanamcheka kwa kumpeleka Anna shuleni na kuingia gharama zote hizo. Pia ananiambia kuhusu Mama yake kufanya kazi zaidi ili masuala ya nyumbani aweze kuyafanya yeye ili kumsaidia mumewe ambaye pesa yake karibia yote alikua akilipia elimu ya Binti yake.
Mama Anna pia ananisimulia humu jinsi ambavyo aliposwa alipokua kidato cha tano na mchumba ilibidi amsubiri mpaka alipomaliza Chuo Kikuu. Nili enjoy kila sekunde ya maongezi haya ambayo kwa kiasi kikubwa naamini yatakua na faida kwetu sote. Ananihadithia pia jinsi ambavyo alienda Sweden na mumewe ambayo alikua huko kikazi na jinsi ambavyo alipata nafasi ya kusoma Chuo Kikuu BURE na ni nafasi ambayo aliipokea kwa mikono miwili na kuhakikisha hafanyi makosa.
Mama Anna ameshaifanyia Dunia hii mambo tele ya kimaendeleo wakati akifanya kazi zake UN na baada ya hapo alirudi nyumbani na kukifanya kazi Chama cha Mapinduzi kama Mbunge wa Muleba Kusini na Waziri wa Ardhi, nyumba na Maendeleo ya makazi. Hapo kwenye uwaziri sasa… Kulikua na mengi yaliyotokea wakati yeye yuko kwenye cheo hiko na ambayo kwa ki ufupi tu tuliyajadili kwenye meza yetu. Mama Anna yuko na Respect ya hali ya juu kwa Rais wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye kwa kiasi kikubwa alimfanya Professor Tibaijuka arudi nyumbani na kulifaidisha Taifa na yale alojifunza wakati anafanya kazi huko kwenye Umoja wa Mataifa.
Yangu matumaini utaokota kadhaa kwenye maongezi yetu haya na kwa kiasi flani yatakusaidia kwenye maisha yako. Tafadhali enjoy pia.
Love,
Salama.
Support us through anchor.fm/yahstonetown/support
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahStoneTownSubs
Listen our Podcast on
Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link bit.ly/GooglePodcastSalamaNa
Audiomack Link bit.ly/YahStoneTownAudioMack
‪KZread Link bit.ly/KZreadSalamaNa
Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
Follow:
Twitter: / yahstonetown
Instagram: / yahstonetown
Facebook: / yahstonetown
Channel Administered by Slide Digital
Instagram: slidedigitaltz

Пікірлер: 141

  • @johnwilfred3920
    @johnwilfred3920 Жыл бұрын

    Huyu Professor ana madini mengi sana. Kichwa chake ni hazina.

  • @aivanandrea2160
    @aivanandrea2160 Жыл бұрын

    Uongozi sio kuongezeka vyeo..bali kuwasaidia watu kufikia malengo yao🙌🙌🙌🙌

  • @liliankilave3496
    @liliankilave3496 Жыл бұрын

    I just loved the positivity and the Haya people perspectives😅😅😅😅

  • @mfamauomary7969
    @mfamauomary7969 Жыл бұрын

    Hongera sana da Salama kwa kutuletea huyu bib Anna❤ Yupo sahihi kwa anayoyaelezaaa hongera akee❤

  • @margarethmwampondele7858
    @margarethmwampondele7858 Жыл бұрын

    my role model. good interview.. ...asante sana Salama kwa kubuni kipindi. we love u

  • @wellbrand3415
    @wellbrand3415 Жыл бұрын

    Wow... Just wow... Huyu mama nampenda sana...

  • @kambamazig02024
    @kambamazig02024 Жыл бұрын

    Kudos Prof. nimefurahi sana kukusikia ukiongelea kizazi cha wapigania uhuru, vijana wengi siku hizi wanayachukua haya mambo for granted na wanauona utamaduni wetu kama vile ni kero kwao.

  • @blasioshitsirishibachi9739
    @blasioshitsirishibachi9739 Жыл бұрын

    Watching from Nairobi Kenya. We love you mama. Respect Mungu akuongezee miaka na maisha mema.

  • @swahiliwithZita
    @swahiliwithZita Жыл бұрын

    Our UN habitat way maker. She paved the way for African/Tanzanian women

  • @barbarasara4033

    @barbarasara4033

    Жыл бұрын

    She stole money and akasema pesa ya mboga shame on her

  • @user-bg5kg2bb4j

    @user-bg5kg2bb4j

    Жыл бұрын

    She stolen not but she given hela ya mboga.

  • @AfricaYangu
    @AfricaYangu Жыл бұрын

    I was just thinking how educational system haiendani na ulimwengu wa leo , Natumaini serikali itafanyia hili mabadiliko ili kujikwamua kiuchumi. Well said Mama Tibaijuka 👏

  • @japhetmgema3208
    @japhetmgema3208 Жыл бұрын

    We, academicians, are so proud of you Prof. Anna

  • @sakrypapilon1320
    @sakrypapilon1320 Жыл бұрын

    entreprenuership is an organizational skill, well put!! such a good interview.

  • @twahasuleiman-lo9vl
    @twahasuleiman-lo9vl Жыл бұрын

    Alhamdulillah nimemuelewa na nimejifunza...

  • @prettypretty9745
    @prettypretty9745 Жыл бұрын

    Napenda Sana wakristo wanapotumia neno Alhamdulillah katika njia ya kumshukuru Allah ........... The powerful of Islamic

  • @productuzur7585

    @productuzur7585

    Жыл бұрын

    Sisi hatuna unaguzi wa kidini

  • @charlesluanda9161
    @charlesluanda9161 Жыл бұрын

    One of the best interviews Salama has ever done.

  • @lilianbayekela
    @lilianbayekela Жыл бұрын

    Interview nzuri sana,yaan zaidi ya darasa Nimefurahia kuanzia mwanzo hadi mwisho.Hongera sana Salama na Prof . Anna Tibaijuka

  • @ernestsalla9293
    @ernestsalla9293 Жыл бұрын

    Hongera sana mama Prof Anna. Safari yako ya maisha ni chachu na msukumo chanya kwa watoto wetu wa kike na kiume pia. Endelea kushare uzoefu na maono yako kwa manufaa ya wengi...

  • @kaizamulinda633
    @kaizamulinda633 Жыл бұрын

    I love the fact that she identifies herself more as an academic than a politician. Our current professors are struggling to erase their academic history in favour of political titles! "Umenitoa jalalani"

  • @mwalimuWaZamu

    @mwalimuWaZamu

    Жыл бұрын

    😂😂

  • @eliasmbise4328
    @eliasmbise4328 Жыл бұрын

    Bado nimewahi naombeni like zenu ....

  • @mtaanionlinetv9200
    @mtaanionlinetv9200 Жыл бұрын

    Bonge moja la intervew,🙌🙌

  • @fridageorge2809
    @fridageorge2809 Жыл бұрын

    Nakumbuka shule yangu Jangwani it was 💕 skills za kutosha unatoka umekamilika!

  • @farajalongo4528
    @farajalongo4528 Жыл бұрын

    "Kazi iliyombele yetu ni kubwa kuliko kule tunakotoka." 🙌

  • @msafirikilongo7429
    @msafirikilongo7429 Жыл бұрын

    Ukiangalia nyuma nakujuta Basi hujui ulipo na unapokwenda 🙏🙏

  • @spensiozakato600

    @spensiozakato600

    Жыл бұрын

    ❤❤

  • @braysonminja6744
    @braysonminja6744 Жыл бұрын

    Kabla sijaanza kusikiliza nimeipenda

  • @shijamashima5511
    @shijamashima5511 Жыл бұрын

    Ni enjoy hilo jibu kuhusu mfumo wa elimu

  • @sumayaishengoma4543
    @sumayaishengoma4543 Жыл бұрын

    Mama Anna kichwaa 👏👏👏👏 Asante Salama.

  • @AfiSoul103
    @AfiSoul103 Жыл бұрын

    Jamani...hii vision ya babaake ndio iliyofanya tumjue leo huyu muheshimiwa ANNA....🤗🤗 I wish my father could 😭

  • @ziadamtebwa3712
    @ziadamtebwa3712 Жыл бұрын

    Kwa kweli yupo juu huyu mama asante salama

  • @bettymassanja881

    @bettymassanja881

    Жыл бұрын

    "Leadership is about raising others to achieve their goals". Such a statement can only be given out by rich - hearted people, under the sun, like the Prof. Anna Tibaijuka herself. May the Lord grant her healthful and long life.

  • @siamacha3749
    @siamacha3749 Жыл бұрын

    Prof. Tibajuka ❤ you are the best mama . May God bless you mama

  • @angelmwoleka7892
    @angelmwoleka7892 Жыл бұрын

    Mahojiani bora kuwahi kutokea. Prof. Anna Tibaijuka amefanya kazi kubwa ya kubadilisha mtazamo wa jamii kuhusu kumsomesha binti wa kike. Mungu akupe maisha marefu Profesa.

  • @mchoromohammed6606

    @mchoromohammed6606

    Жыл бұрын

    Hahahaha! Kwani kuna binti wa kiume ?

  • @angelmwoleka7892

    @angelmwoleka7892

    2 ай бұрын

    Ashakum si matusi!

  • @ikupaalimwene6751
    @ikupaalimwene6751 Жыл бұрын

    Mhayaaa

  • @caritastheophil509
    @caritastheophil509 Жыл бұрын

    Hongera sana salama kwa mama yetu, nampenda sana mama tibaijuka, ni role model wangu, namkubali sana

  • @musorobenjamin227
    @musorobenjamin227 Жыл бұрын

    Wahaya ndomana wanafanikiwa sana

  • @edigergabriel3711
    @edigergabriel3711 Жыл бұрын

    Du mama ni noma

  • @premierktg4323
    @premierktg4323 Жыл бұрын

    Very very beautiful interview Mungu ambariki sana Mama Anna Tibaijuka

  • @sophiak8837
    @sophiak8837 Жыл бұрын

    Loved this, i laughed the whole part two section

  • @mwatangalukwili8745
    @mwatangalukwili8745 Жыл бұрын

    My role model,educated woman Prof Anna Tibaijuka.

  • @hamisimahenge5807
    @hamisimahenge5807 Жыл бұрын

    ❤❤❤!!!!!. Guys!!!!, Frankly speaking!!!, This woman is very very 🧠 🧠 intelligent!!!!!.

  • @leonidaleonard9382
    @leonidaleonard9382 Жыл бұрын

    Hongera Mama ana

  • @ralphweston6807
    @ralphweston6807 Жыл бұрын

    Mother anaongea vizur 🙌

  • @Steve3821
    @Steve3821 Жыл бұрын

    Such a lovely interview, my lovely sister Salama you are the best. ❤

  • @jilalamaligisa6298
    @jilalamaligisa6298 Жыл бұрын

    Salama nafuatilia sana kazi zako tangu enzi za Mkasi ila huwa unaboa sana kitu kimoja, una masuali ya kurukaruka mambo muhimu, mfano huyo mama ni mtu muhimu sana kwa kizazi cha leo na vijavyo, wanapaswa kumfahamu kiundani ili waige mazuri yake lakini sasa wewe unaanza na suali eti kuhusiana na kuingia kwenye siasa, kwa nini usiyatazame maisha yake kwa mpangilio mzuri kuanzia wazazi wake, kuzaliwa, makuzi, kusoma, kazi, siasa mpaka sasa, unarukaruka na kuacha mambo muhimu hii sipendi kabisa.

  • @CheupeEceJay

    @CheupeEceJay

    Жыл бұрын

    Anzisha chako usiwe unarukaruka...Nadhani utatisha sana! Pia asante kwa KUFUATILIA SANA!

  • @raymullah
    @raymullah Жыл бұрын

    Interesting interview

  • @cherietigress3109
    @cherietigress3109 Жыл бұрын

    one of the best interview 🙌 👌 Tunajivunia mama Anna Tibaijuka

  • @faudhiasalum7279
    @faudhiasalum7279 Жыл бұрын

    Awesome 👌🏽

  • @barakakusa7606
    @barakakusa7606 Жыл бұрын

    Nimeipenda hii👍

  • @kilamiko8299
    @kilamiko8299 Жыл бұрын

    Salama! you are the best!

  • @magnusmutayoba8040
    @magnusmutayoba8040 Жыл бұрын

    Interview kali sana 👏👏

  • @Bob-kz2ql
    @Bob-kz2ql Жыл бұрын

    Hatari sana mama kasoma hadi kasoma tena…NICE one Prof, too bad ckhz tumebaki na ma Prof wa kupost picha za kubenjua makalio tu insta

  • @aairraahseif5648

    @aairraahseif5648

    Жыл бұрын

    👏👏👏👊👊

  • @jooepaullas791

    @jooepaullas791

    Жыл бұрын

    😅😅😅

  • @israelkisaila8401

    @israelkisaila8401

    Жыл бұрын

    BOB HAHAHA

  • @barbarasara4033

    @barbarasara4033

    Жыл бұрын

    Pesa ya mboga imemuharibia

  • @mohamedothman5792

    @mohamedothman5792

    Жыл бұрын

    Kusoma kwake kumesaidia nini taifa zaidi ya kujinufaisha yeye mwenyewe

  • @frankmushi4846
    @frankmushi4846 Жыл бұрын

    Bonge ya interview 🙌

  • @richardkosianga8981
    @richardkosianga8981 Жыл бұрын

    one of the best interview hongera sanaa salama

  • @margepeter6697
    @margepeter6697 Жыл бұрын

    My rolemodel 😍😍😍

  • @farajalongo4528
    @farajalongo4528 Жыл бұрын

    Ability Vs Willingness 🙌🙌

  • @joviangeofrey6918
    @joviangeofrey6918 Жыл бұрын

    Iwe bojooooo

  • @albs1448

    @albs1448

    Жыл бұрын

    Waitu oliyo bojo?

  • @maureenmpate5941
    @maureenmpate5941 Жыл бұрын

    Nice interview

  • @gastokakiziba7871
    @gastokakiziba7871 Жыл бұрын

    Prof yuko vzr sana,kuna vijana weng sana wanadgree mtaani lakin wamefungua migahawa

  • @castomhadisa9222
    @castomhadisa9222 Жыл бұрын

    If professor you read these comments,, I love you from my heart

  • @justinejackson1731
    @justinejackson1731 Жыл бұрын

    Dah! Akili kubwa...kumuelewa unatakiwa kukaa kwa kutulia sana, atema madini mda wote.

  • @makiniautospare2648
    @makiniautospare2648 Жыл бұрын

    Inasikitisha sana sihasa inavyowageuza wasomi wetu kuwa wabinafsi waliopitiliza na kuweka taaluma zao kando.

  • @christopheritambo1315
    @christopheritambo1315 Жыл бұрын

    Nilisoma story za huyu mama I guess form three or form four

  • @antonyjosephatkaiza2565
    @antonyjosephatkaiza2565 Жыл бұрын

    mafanikio ni product ya teamwork na mazingira 👏

  • @stanymccary7136
    @stanymccary7136 Жыл бұрын

    Mama kichwa sana, sema Siasa zilitaka kumuharibia IQ yake lkn mtu ambaye ni msomi kweli na ni icon ya wahaya

  • @sangomamourice3539
    @sangomamourice3539 Жыл бұрын

    Wakurungwa mmeshawahi

  • @niriacatering172
    @niriacatering172 Жыл бұрын

    Prof upo vizuri sanaa

  • @alexandermutakha882
    @alexandermutakha882 Жыл бұрын

    Kazi iendelee

  • @jescajoseph1072
    @jescajoseph1072 Жыл бұрын

    👏👏👏❤

  • @ulludots
    @ulludots Жыл бұрын

    Interview nzuri sana

  • @ashirafmgonanze-pl6qf
    @ashirafmgonanze-pl6qf Жыл бұрын

    First

  • @vediowkiritasi3163
    @vediowkiritasi3163 Жыл бұрын

    Very nice Interview

  • @faisalihamudi9206
    @faisalihamudi9206 Жыл бұрын

    Mama kuna Newyork city kule Muleba

  • @michaelcyprian6733
    @michaelcyprian6733 Жыл бұрын

    Miongoni mwa Interviews bora kabisa.

  • @roberteliezer9576
    @roberteliezer9576 Жыл бұрын

    powerfull

  • @CaAidan
    @CaAidan Жыл бұрын

    I underestimated this mama🙌🙌🙌

  • @arnoldkimbory485
    @arnoldkimbory485 Жыл бұрын

    Interview nzur sana

  • @nambuacassandramlaki3516
    @nambuacassandramlaki3516 Жыл бұрын

    Love you Mama.

  • @michaelwaryoba4904
    @michaelwaryoba4904 Жыл бұрын

    Huyu mama Yuko vizuri sana .

  • @emmanueltibahwa2615
    @emmanueltibahwa2615 Жыл бұрын

    Life is what you make it!

  • @erickmsigwa
    @erickmsigwa Жыл бұрын

    Wapili

  • @alexandermutakha882
    @alexandermutakha882 Жыл бұрын

    Wazazi walikuwa na maono kweli.

  • @jojigeorige1056
    @jojigeorige1056 Жыл бұрын

    Natamani Salama siku moja nae amhoji Salama!... nimependa sana hii interview

  • @jojigeorige1056

    @jojigeorige1056

    Жыл бұрын

    Pia nimejifunza mengi sana. With my headphones on nimejikuta na nod mara nyingi kupiliza. Mama katema madini aisee

  • @abuusirleh8196
    @abuusirleh8196 Жыл бұрын

    Mjanja mjanja

  • @godfreypeter9265
    @godfreypeter9265 Жыл бұрын

    Ameongea ki2 ambacho serikali kwa ujumla inatakiwa kuzingatia sana juu ya elimu

  • @yuliahenry3383
    @yuliahenry3383 Жыл бұрын

    Nice MAMA

  • @ludovickbenjamin6104
    @ludovickbenjamin6104 Жыл бұрын

    uyu mama anajielewa sana.

  • @lutfiayussuf4729
    @lutfiayussuf4729 Жыл бұрын

    The best interview ever❤ #SALAMA NA PROF ANNA TIBAIJUKA

  • @abelchacha5977
    @abelchacha5977 Жыл бұрын

    Mama hauna ha mjakazi angalau........ningekua na wewe ningefaidika sana. Napenda ushauri wako, napenda maamuzi yako.

  • @damsonwilson5202
    @damsonwilson5202 Жыл бұрын

    Huyu Mama Ana Akili sana

  • @bestantony7917
    @bestantony7917 Жыл бұрын

    Duu Prof Akili kubwa

  • @abdulmajidchum9085
    @abdulmajidchum9085 Жыл бұрын

    Tunaomba utuletee zimbwe junior Mohamed hussein

  • @AdamSaffi211
    @AdamSaffi2117 ай бұрын

    Wabongo tulivyo wapumbafu, tumeisha sahau yote. Accepting stolen money is a crime, whether you know it or not. Bongo hata hakushutakiwa. Mwongo, mwizi just like any politician! Asitidanganye hapa. I can’t believe how she paints herself as a saint. Do we know other monies she was given by corrupt mbwa, no, we will never know!

  • @stevesundu1671
    @stevesundu1671 Жыл бұрын

    Tunataka interview na zumaridi!

  • @g-abbastechnology1818
    @g-abbastechnology1818 Жыл бұрын

    kohoa upate tonge nan mwingine kaiona iyo

  • @annakweka421
    @annakweka421 Жыл бұрын

    Anna

  • @aggreyenock1221
    @aggreyenock1221 Жыл бұрын

    MHAYA

  • @musorobenjamin227
    @musorobenjamin227 Жыл бұрын

    Hii interview nitaitunza kwa ajili ya mwanangu wa kike

  • @julianamushi3392
    @julianamushi3392 Жыл бұрын

    Namuona ebitoke😆😆ni utani jmn sina mwanasheria

  • @AdamSaffi211
    @AdamSaffi2117 ай бұрын

    Not she is a crook just like any politician in Bongo. Her, bishops et al, was given a lot of stolen money. When she got caught, she claimed she gave the money to a private school as a gift.

  • @mosesmashili4969
    @mosesmashili4969 Жыл бұрын

    Dada Salama, Boresha kwenye Uulizaji wa Maswali... unauliza maswali laini sana naweza sema hivyo, tunahitaji kujifunza zaidi.

  • @barakakusa7606

    @barakakusa7606

    Жыл бұрын

    Onesha mfano wa maswali magumu ambayo ulitamani angeuliza.

  • @hellendaniel3809

    @hellendaniel3809

    Жыл бұрын

    Khaaaa wewe sio mfuatiliaji salama ana uzoefu sio wa jana ni longtime ago in Bethlehem

  • @mosesmashili4969

    @mosesmashili4969

    Жыл бұрын

    @@hellendaniel3809 Salama nimeanza kumfatilia tangu yupo Chanel 5 MKASI, ni long time namfahamu kuliko Unavyodhani... Ebu mfatilie Stanislaus Lambat wa Dar24 ndio utanielewa ni nini namaanisha.

  • @barbarasara4033

    @barbarasara4033

    Жыл бұрын

    Exactly Ile scandal ya wizi ilimshusha kiasi gan mpaka akasema pesa ya mboga. Nilitaka kufahamu haya mengine Utopolo tu

  • @abdulsataribashiri8300

    @abdulsataribashiri8300

    Жыл бұрын

    Hakuna muulizaji Wa maswali magumu hapa bongo kama huyu Salama wengne wte hamna kitu

  • @King_Of_Everything
    @King_Of_Everything Жыл бұрын

    🇹🇿🇹🇿🇹🇿✌️👊

  • @TheParty.
    @TheParty. Жыл бұрын

    👏👏👏👏👏👍👍👍👍

Келесі