Msaada toka kwa kamati ya wanawake dini mbalimbali Dodoma kwa ajili ya waathirika wa mvua za tope.

Viongozi wa Kamati ya wanawake wa dini mbalimbali Mkoa wa Dodoma wamekabidhi mahitaji mbalimbali muhimu katika ofisi za CCT Dodoma kwa ajili ya kusafirishwa kwenda kwa waathirika wa mafuriko,wilayani Hanang, Mkoani Manyara.
Askofu. Mary C. Madelemo wa Kanisa la Pentecostal Holiness Association Mission Tanzania( PHAMT) ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya wanawake wa Dini mbalimbali Mkoa wa Dodoma amesema wanawake waliguswa na athari zilizotokea kwa wakazi wa Hanang baada ya mafuriko,hivyo kwa moyo wa upendo na wa huruma waliamua kukusanya mahitaji mbalimbali kama Sabuni ,Nguo na Vyombo kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa mafuriko wilayani Hanang,mkoani Manyara.
Mchungaji David Kalinga ,Afisa Programu wa mahusiano ya dini mbalimbali-CCT akipokea mahitaji hayo amewashukuru na kuwapongeza wanawake hao kwa moyo wao wa huruma na upendo wa kuwasaidia wenye uhitaji.
CCT Inaendelea kupokea mahitaji muhimu kutoka kwa wadau mbalimbali na vitu vyote vinavyokusanywa vitawasilishwa rasmi kwa waathirika wa mafuriko wilayani Hanang, Mkoani Manyara tarehe 26/01/2024.

Пікірлер: 1

  • @madamhilaliaphilipo7551
    @madamhilaliaphilipo75515 ай бұрын

    Yesu awabariki sana kwakweli