Kwa nini Kanisa la Mungu Tanzania liliitwa hivo? Nani mwanzilishi?

Kanisa la Mungu Tanzania ni moja ya Makanisa Wanachama wa CCT, Makao makuu ya Kanisa hili yapo wilayani Babati, Mkoani Manyara, Tangu Kanisa hili limeingia nchini mnamo mwaka 1959 limeendelea kufanya kazi ya kuihubiri Injili na kuendelea kuenea katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu.
Mara baaada ya Ibada ya Jumapili ya leo iliofanyika katika Kanisa la Mungu Tanzania Babati Mjini na kuhudhuriwa na baadhi ya watumishi wa CCT kutoka makao makuu Dodoma, Mchungaji Daudi Garang ambaye ni Mchungaji kiongozi wa Kanisa la Mungu Tanzania Babati Mjini na Katibu Mkuu msaidizi wa Kanisa hilo aliwakaribisha na kuwashukuru baadhi ya watumishi wa CCT kwa kushiriki Ibada hiyo pamoja na kuwakumbuka waathirika wa Maafa ya mafuriko wilayani Hanang.
Mch.Boniface Majengo Mkuu wa Chuo Cha Biblia kinachomilikiwa na Kanisa la Mungu Tanzania ameeleza kwa undani kuhusu historia ya Kanisa la Mungu Tanzania , Imani na utaratibu wa Ibada wa Kanisa hilo. Akiendelea kuelezea historia ya Kanisa hilo aliyekuwa Mhazini Mkuu wa kwanza na mmoja ya waasisi wa Kanisa hilo.Mch.James Reuben Kimbalambala alisema Kanisa hilo lilijiunga na Jumuiya ya Kikristo Tanzania CCT kwa lengo la kuungana na Makanisa mengine na kuwa na nguvu ya pamoja katika kueneza ufalme wa Mungu pia Kushirikiana na Serikali kupitia Jumuiya hii ili kutatua changamoto mbalimbali katika jamii , pia amesema tangu Kanisa hilo limejiunga na CCT limefaidika katika mambo mengi na wamekuwa wakishirikiana vizuri na viongozi wa Makanisa mengine wanachama ya CCT.

Пікірлер