MBUZI ALIWA UWANJANI MCHANA KWEUPEEE BAADA YA USHINDI

NA ALBERT G. SENGO/MWANZA
Hatimaye timu ya kandanda ya Elias Garage fc wametawazwa kuwa Mabingwa wa Michuano ya Mbao fc Kombe la Mbuzi mara baada ya kuwatungua bao moja sufuri wababe wa Ilemela Wakulungwa Fc katika mchezo wa fainali uliopigwa leo katika uwanja vya Mbao Sabasaba jijini Mwanza.
Pamoja na zawadi ya Mbuzi mnyama Jembe fm ilikabidhi zawadi ya mpira wenye hadhi ya michuano ya ligi Kuu uliotolewa na Duka la vifaa vya michezo la Makilagi Sports Wear, sanjari na pumpu yake.
Jicho la Sports Ripoti lilikuwa pale na mwanamichezo wetu Albert G Sengo, anashuka na taarifa zaidi.....

Пікірлер