Kinachoendelea mgomo wafanyabiashara Mwanza, adai kunyimwa unyumba

Ni maumivu. Ndivyo unavyoweza kusema wakati mgomo wa wafanyabiashara wa maduka jijini Mwanza ukiingia siku ya tatu huku waendesha maguta, magari ya mizigo, mamalishe na makuli wakihofia ndoa na familia zao kusambaratika.
Juni 24, 2024, wafanyabiashara jijini Dar es Salaam walitangaza mgomo na kufunga maduka yao kushinikiza Serikali kuondoa utitiri wa kodi katika biashara zao, baadaye mgomo huo uliibukia jijini Mwanza, Mbeya na Dodoma kisha Mtwara, Iringa, Arusha, Songwe na Njombe.
Akizungumza na Mwananchi Digital leo, Alhamisi Juni 27, 2024, Dereva wa gari dogo la mizigo Mtaa wa Liberty jijini humo, Ndaluka Kamata amesema kabla ya mgomo huo alikuwa anapafa hadi Sh50, 000 kwa siku, lakini sasa mambo yamebadilika anakosa hata Sh5,000 na hivyo kushindwa kuihudumia familia yake.
Ndaluka amesema kutokana na kupungua kipato, ameshindwa kukidhi mahitaji ya familia yake kwa chakula jambo linalosababisha anyimwe hadi unyumba.

Пікірлер: 1

  • @giftlema8296
    @giftlema829625 күн бұрын

    Mmmmh!!!!😮

Келесі