"HAKUNA KUPEWA MRADI MWINGINE..!", BASHUNGWA AWAONDOA WATAALAMU WOTE WA BARABARA YA KIBAONI - MLELE

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameagiza kuondolewa kwa wataalam wote wanaosimamia ujenzi wa Barabara ya Kibaoni - Sitalike, sehemu ya kwanza ya Kibaoni - Mlele (km 50) kwa kiwango cha lami kutokana na ujenzi wa mradi huo kusuasua na utekelezaji wake kuwa nyuma kwa asilimia 23.71.
Ameagiza kuondolewa kwa Wataalam wote wa Mhandisi Mshauri wa Mradi Kampuni ya Crown Tech, Msimamizi wa Mradi kutoka Makao makuu ya TANROADS, Eng. Ramadhan Myanzi pamoja na Msimamizi wa Mradi Mkoa wa Katavi, Eng. Albert Laizer.
Bashungwa ametoa agizo hilo Aprili 08, 2024 mkoani Katavi wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Kibaoni, Mkoani Katavi mara baada ya kukagua mradi huo ambao kwa sasa umefikia asilimia 14.7 na kutoridhishwa na kasi ya usimamizi na utekelezaji wa mradi huo.

Пікірлер: 16

  • @alfinmbilinyi5985
    @alfinmbilinyi59853 ай бұрын

    Yeah!🇹🇿kwa staili hii Tanzania itaendelea.safi sana waziri.

  • @williammwamalanga1065
    @williammwamalanga10652 ай бұрын

    Hongera sana sana waziri

  • @amanafi1288
    @amanafi12883 ай бұрын

    Bashungwa upo juu sana hongera sanaa.. Big up

  • @user-su3lw1om2h
    @user-su3lw1om2h3 ай бұрын

    Kaka bashungwa nakubari njoo nadodo uwanja wandege msalato tunanyanyasika

  • @henryndosi2002
    @henryndosi20022 ай бұрын

    Mzee mwenyewe ni mpole sana hafai

  • @ShaibWazir
    @ShaibWazir3 ай бұрын

    Namna hii nimependa utendaji wako waziri.

  • @jamalimussa4928
    @jamalimussa49283 ай бұрын

    Piga kazi Jembe

  • @aminitu3766
    @aminitu37663 ай бұрын

    Duh! Safi mkuu watu hawaamini kwamba Mambo hamebadilika wataelewa tu !

  • @naligiatomaso5006
    @naligiatomaso50063 ай бұрын

    Hao Chico mkuu Hana maajabu hapo wameshakuwa waswahili

  • @jackmabirangacharles9398
    @jackmabirangacharles93983 ай бұрын

    Mheshimiwa Bashunga pls Tunakuomba sana Pamoja na Kwamba unapambana huko Mikoani naomba nikuulize pale Muhimbili zile Barabara ya kuingia Muhimbili Dar Mjini kuna Chamoto gani? Maana pale wagonjwa wazazi wanaletwa na Ambulance 🚑 wako hoi yale Mashimo waziri mkuu alitoa maagizo , Makam wa Rais alitoa Maagizo tataizo liko wapi? Matengenezo

  • @user-wm1hq9zf2x
    @user-wm1hq9zf2x3 ай бұрын

    Tatizo ni makampuni ya usimamizi ndio changamoto.

  • @evancykashaga6576
    @evancykashaga65762 ай бұрын

    Mijitu nimijizi mpaka basi alafu wananchi wana pelekeshwa kwa vitu vidogo tu yani

  • @user-cg1vd5jr8t
    @user-cg1vd5jr8t3 ай бұрын

    Kipande Cha SGR MAKOTOPORA ISAKA KAKA KIMELALA UJE UJIONEE

  • @bharyasarbjit1187
    @bharyasarbjit11873 ай бұрын

    Mhe una sema local contractor Babaishazi umpe hawa Bado Utaona Mambo Zaidi. Uli nyima sisi Mpwapwa Gulwe umpe Hawa. We are not interested now wasting time of local contractor.

  • @MasterOil-qm6vw
    @MasterOil-qm6vw2 ай бұрын

    Hawa watu hawa wanatakiwa wafungwe jela sasa mlisomea upuuzi gani huko shule bora hata wapewe watu darasa la saba yaan watu ni wajinga mtu huwez kusimamia mambo na eti umepoteza ada zako kusomea kitu hiko kweli mimi najiamini kwa kule kusimamia msumamo wangu wa kwamba vyeti hainifanyi nimpe mtu kazi

  • @IssaAbdallah-rt2sh
    @IssaAbdallah-rt2sh2 ай бұрын

    Barabara ya pangani tanga inamiaka.15 haimaliziki sioni.watu.wakihoji.chochote.wala mawaziri ambao niwakazi.wa tanga wamekaa kimya sijui wanamatatizogani

Келесі