GIVE ME THAT MOUNTAIN - PASTOR SUNBELLA KYANDO

Ойын-сауық

Kalebu anamkumbusha Yoshua kuhusu ahadi na kiapo alichoapa Musa kwa Mungu kuwa atampa nchi baada ya kuingia Kanaani kwa ajili ya wema na utimilifu wake kwa za Mungu.Kabla ya kuingia Kanaani Musa alituma wapelelezi wakapeleleze kwenye hiyo nchi(Kanaani) na wapelelezi kumi walikuja na taarifa mbaya kasoro Yoshua na Kalebu peke yao,na kwa sababu hiyo Musa akamuapia Kalebu kwa Mungu kuwa watakapoingia Kanaani kuna nchi atampa.
Musa hakufanikiwa kuingia Kanaani kwa sababu alimkosea Mungu na Mungu akamwambia kuwa hatoingia ile nchi.Wakati Kalebu anaahidiwa ahadi hii alikuwa na umri wa miaka 40 na ikapita miaka 45 zaidi bila yeye kupewa hiyo nchi.
Wakati huo watu wa Yuda walikuwa wamemfuata Yoshua kwa sababu kuna maeneo walikuwa wakiyataka,Kalebu naye akaenda na akamkumbusha Yoshua juu ya ahadi aliyoahidiwa maana wakati Musa anaahidi Yoshua naye alikuwepo.
Na Kalebu hakuishia hapo,alimwambia Yoshua eneo analolitaka,nchi iliyopo katika mlima Horebu.Ukisoma mstari wa 12 utaona kitu kikubwa sana;Kalebu anasema kuwa kama ambavyo alikuwa na nguvu alipopewa ahadi hii akiwa na miaka 40 vivyo hivyo bado ana nguvu za kupigana vita hata katika miaka hiyo 85 aliyonayo.Kwa maana nyingine ni kuwa, kutokana na ahadi ambayo ipo kwenye maisha yake mwili wake haukutakiwa kukua na kuishiwa nguvu maana atazihitaji kwenye kumiliki ahadi yake.Mungu ilibidi aende kinyume na kanuni za mwili kuwa hata katika miaka 85 aliyonayo bado ana nguvu za kupigana vita na jeshi na akashinda.
Mungu anapokupa ahadi hata kama kanuni ya mwili hairuhusu bado Mungu yupo juu ya kanuni zote.Kama una ahadi ya kupata mtoto kwenye maisha yako,hata kama kanuni ya mwili inasema umri wako umeenda sana na huwezi tena kushika ujauzito lakini kwa Mungu hakuna kisichowezekana.
Lakini pia Kalebu alijua kuwa kuwa na nguvu za mwili tu haitoshi kushinda vita,alihitaji pia Neno la Mungu kutoka kwa Yoshua.Neno la Mungu huwa limebeba nguvu lakini pia neema ya kukusaidia,kuwa na nguvu bila kuwa na Neno la Mungu bado hutoweza kushinda.
#PastorSunbella#GiveMe#ThatMountain

Пікірлер: 30

  • @deniskimario9288
    @deniskimario92882 жыл бұрын

    Nimesoma hapo last week, ila sikupata huu ufunuo. Asante Yesu Kristo, niko chini ya huyu mtumishi wako

  • @petermunuo1657
    @petermunuo1657 Жыл бұрын

    I received mountain in the name of Jesus... Amen

  • @linahliz2130
    @linahliz21304 ай бұрын

    Hallelujah hallelujah hallelujah glory to God

  • @user-vv9yh3dn5q
    @user-vv9yh3dn5qАй бұрын

    Halaluyaa❤

  • @prospernyoni8326
    @prospernyoni8326 Жыл бұрын

    Be blessed alot Pastor a really appreciate you

  • @bennamuchau6487
    @bennamuchau64872 жыл бұрын

    Napokea mlima wangu ahadi za Mungu juu ya maisha yangu katika jina la Yesu Kristo Mwana Mungu aliye hai.

  • @veronicakazungu2395
    @veronicakazungu23952 жыл бұрын

    Amen nabarikiwa mimi maana napokeq mulima wangu

  • @mungajoas3343
    @mungajoas3343 Жыл бұрын

    AMEN

  • @maryandason1815
    @maryandason18152 жыл бұрын

    Dad Sanbella..Lin wa mikoan tukujee ?? Reality Christ.siku nitakayokanyaga madhabahu ya Reality Christ.ndo siku yangu ya kukutana live na YESU.. barikiwa Sana bishop Sanbella 🙏🙏. YESU nisaidieee niwezeshe kuupta mlma wangu.

  • @g.karathaofficial666
    @g.karathaofficial6662 жыл бұрын

    No comment but nguvu ya Mungu iko ndani yako,na ndivyo roho amenionyeshea hivyo.I receive my mountain.

  • @annkauri7406
    @annkauri74062 жыл бұрын

    My pastor may heavenly father bless you uishi miaka mingi,we need this reality ,your teaching has changed me completely.Ann from kenya. baba be blessed

  • @faudhiasalum7279
    @faudhiasalum72794 ай бұрын

    Yeah dady 😢😢

  • @ThomsonTumain
    @ThomsonTumain2 жыл бұрын

    My best teacher for this time

  • @priscaadongo1922
    @priscaadongo19222 жыл бұрын

    Tamka neno juu ya maisha yangu mtumishi Sanbela ukweli kabisa yatakua

  • @sabrinawanyika4802
    @sabrinawanyika48022 жыл бұрын

    Nakushuru mtumishi wa mungu ume nifuza megi sikuyajuwa

  • @jinamuluba6799
    @jinamuluba67992 жыл бұрын

    mtumishi umenibariki sana ubarikiwe saanaa

  • @gloryjohn343
    @gloryjohn3437 ай бұрын

    🙏🙏

  • @priscaadongo1922
    @priscaadongo19222 жыл бұрын

    I receive my maintain in Jesus mighty name AMEN thanks

  • @fionaalice9509
    @fionaalice95092 жыл бұрын

    Amen 🙏🙏 nipokea mlima wangu

  • @samsonmkumbo4793
    @samsonmkumbo47932 жыл бұрын

    Mtumishi njoo na Moshi tunakusubiri kwa ham kubwa Sana 🙏

  • @elishasoka6692
    @elishasoka66922 жыл бұрын

    I receive my miracle in Jesus name

  • @rodrickmasawe2948
    @rodrickmasawe29482 жыл бұрын

    I received my mountain in jesus name

  • @christabelmarembo421
    @christabelmarembo4212 жыл бұрын

    Thank you Jesus 😭😭😭😭

  • @christinesavai884
    @christinesavai8842 жыл бұрын

    Give me that mountain

  • @chantalmwipata8820
    @chantalmwipata88202 жыл бұрын

    Amen 🙏 🙏

  • @daddydadamtabo998
    @daddydadamtabo9982 жыл бұрын

    Amena Amena

  • @scholarnduku8887
    @scholarnduku88872 жыл бұрын

    I receive my mountain in Jesus Name 🙏.Nimebarikiwa sana.

  • @sabrinawanyika4802
    @sabrinawanyika48022 жыл бұрын

    Kutoka kwa Islam sirahisi lakini sasa nisha juwa kupambana kiroho

  • @adamwapiliadamwapili5698
    @adamwapiliadamwapili56982 жыл бұрын

    😭😭😭😭😭😭🙏

  • @annstersianganga6772
    @annstersianganga67722 жыл бұрын

    Amen napokea mlima wangu in Jesus Mighty Name. Kama Caleb sijakata tamaa miaka yaweza kuwa imeenda ndio lakini mlima pia upo. Eee Bwana kupitia mlima huu nitakua baraka kwa wengi nitakuletea utukufu ,Amina

Келесі