16,646 wachaguliwa kujiunga vyuo vya afya, 1,842 wakosa sifa

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Nactvet) imetangaza matokeo ya awamu ya kwanza kwa walioomba kujiunga na programu za Afya na Sayansi Shirikishi kwa mwaka wa masomo 2024/25 huku waombaji 1842 wakikosa sifa.
Waombaji 16,646 wamechaguliwa kujiunga kwenye vyuo 221 vinavyotoa programu mbalimbali za afya na sayansi shirikishi.
Hao ni kati ya waombaji 24,629 waliowasilisha maombi kupitia mfumo wa udahili wa pamoja (CAS).
Akitangaza matokeo hayo ya awamu ya kwanza leo Julai 11, 2024 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Udahili, Utahini na Utunuku wa Nactvet, Dk Marcelina Baitilwake amesema kati ya waombaji 24,629 ni 23,503 ndiyo walikamilisha maombi yao kwa kuchagua vyuo na programu walizopenda.
Amesema, waombaji wengine wenye sifa lakini hawakuchaguliwa ni wale walioomba programu tofauti na sifa walizonazo.
Amesema awamu ya tatu itakuwa ni Septemba na dirisha litafungwa Septemba 28.

Пікірлер

    Келесі