Wasimulia madawa, skanka yanavyovunja ndoa Tanga, Bangi ikiendelea kuwa janga nchini

Ripoti ya dunia ya dawa za kulevya ya 2024 iliyozinduliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na dawa za kulevya na uhalifu, (UNODC), inasema idadi ya watumiaji wa dawa za kulevya ulimwenguni imeongezeka na kufikia watu milioni 292 mwaka 2022 ikiwa ni ongezeko la asilimia 20 katika kipindi cha miaka 10.
Akizindua ripoti hiyo jijini Vienna Austria Mkurugenzi Mkuu wa UNODC, Ghada Waly ameeleza kuwa matumizi ya bangi yameendelea kutumika zaidi duniani kote ambapo kuna watumiaji bangi milioni 228.
Ripoti hiyo pia imesema uzalishaji wa kokeini umeweka rekodi mpya ya juu ya uzalishaji wa tani 2,757 kwa mwaka 2022, ikiwa ni ongezeko la asilimia 20 zaidi tangu mwaka 2021.
Hata hivyo, nchini Tanzania kwa mujibu wa taarifa ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ya mwaka 2023, imesema jumla ya tani 1,965.34 za dawa za kulevya zilikamatwa kwa mwaka 2023 pekee ikiwa ni karibu mara saba zaidi ya kiasi kilichokamatwa tangu mamlaka hiyo ianzishwe mwaka 2017.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa bangi iliendelea kukamatwa kwa wingi nchini ikiwa na tani 1,757.56 ikifuatiwa na mirungi tani 202.74, heroni tani 1.31 na kokeni kilo 3.04.

Пікірлер

    Келесі