WAMEYAKANYANGA | WAZIRI MKUU AINGILIA KATI MAUAJI YA MTOTO ASIIMWE, ATOA MAELEKEZO MAZITO

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameielekeza Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, mara upelelezi utakapokamilika, kuwafikisha mahakamani mara moja watuhumiwa wote waliohusika na mauaji ya mtoto Asiimwe Novath aliyekuwa na umri wa miaka miwili na nusu mkoani Kagera, ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaofikiria kufanya vitendo kama hivyo.
Waziri Mkuu ametoa maelekezo hayo bungeni jijini Dodoma leo asubuhi alipokuwa akiwasilisha tamko la Serikali kuhusu ulinzi wa mtoto ambapo amewataka wananchi kuachana na imani potofu au mizaha inayolenga kuaminisha kuwa viungo vya watu wenye Ualbino vinaweza kuwaletea utajiri.

Пікірлер: 7

  • @abuushakiraddausiy8666
    @abuushakiraddausiy866611 күн бұрын

    Nawaombeni sanaa serekeli Sheria ifuate mkondo wake ikiwapendeza wapigwe risasi hadharanii...ili iwefundisho kwa wenyetabia kama hii ..kunyonga kwa siir haitofundishaa sana....twaomba Sheria ifuate mkondo wake....

  • @michaelndilima6210
    @michaelndilima621016 күн бұрын

    Shida watu sasa wanafiria pesa zaidi kuliko mwenyezi mungu.

  • @ChainaDamian
    @ChainaDamian4 күн бұрын

    Mungu awape nguvu jeshi la polisi

  • @NaomiCharles-bb8md
    @NaomiCharles-bb8md4 күн бұрын

    Mh raisi bola ulivyo chukua atua ya kutatsfuta aki ya uyo bint ashmwe 🙏

  • @uwawatatanzania3243
    @uwawatatanzania32438 күн бұрын

    Wapewe Adhabu kali sana ikiwemo ya kukatwa kiungo kimoja kimoja hadi kufa, hili litakuwa fundisho na kwa wengine wenye Tabia kama hii:

  • @niahofficial7750
    @niahofficial775016 күн бұрын

    Agizo limewafika

  • @edithlameck8170
    @edithlameck817013 күн бұрын

    Mbona nguvu hiyobya kuwapata watuhumiwa haikutumika kumtafuta mtoto? Nina imani nguvu na jitihada za kumtafuta zingefanyika kwa nguvu hiyo basi mtoto angepatikana na kuokolewa akiwa hai. Jeshi la polisi lijitafakari.......

Келесі