Viongozi Tana River wameirai serikali kutenga pesa za kukarabati shule zilizoharibiwa na mafuriko

Viongozi katika kaunti ya Tana River wameirai serekali kuu kutenga fedha za kufadhili ukarabati wa miundomsingi katika shule zilizoharibiwa na maji ya mafuriko.
Akizungumza katika shule ya msingi ya Makere, eneo bunge la Galole, Mbunge wa Galole Said Hiribae amesema kuwa itakuwa vigumu kutimiza wito wa rais wa kujenga shule zilizoharibiwa na mafuriko endapo pesa za dharura hazitatengwa katika bajeti ya mwaka 2024/25. Zaidi ya wanafunzi 3,000 katika eneo bunge hilo kufikia sasa hawana pa kuendeleza masomo yao.

Пікірлер