Msigwa na CCM lilikuwa suala la Muda tu, Lema, Mrema, Viongozi Chadema wafunguka

Lilikuwa suala la muda kwa Mchungaji Peter Msigwa kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Ndivyo unavyoweza kueleza baada ya kada huyo wa zamani wa Chadema kutimkia katika chama hicho tawala.
Msigwa alitambulishwa kuwa mwanachama mpya wa CCM jana mbele ya wajumbe wa halmashauri kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho, katika kikao kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan.
Uamuzi wa mwanasiasa huyo umethibitisha tetesi zilizokuwa zikiibuliwa mara kwa mara na wadau zikimhusisha Msigwa na CCM, tangu enzi za utawala wa Hayati John Magufuli.
Kwa mujibu wa wanazuoni na wanasiasa, uamuzi wa Msigwa kuihama Chadema na kujiunga na CCM ulitarajiwa, kutokana na mienendo yake ndani ya chama hicho cha upinzani na kauli zake za hivi karibuni.
Mei mwaka huu, wakati anatangaza kukata rufaa kupinga matokeo ya uchaguzi wa Kanda ya Nyasa ulimtupa nje kwenye nafasi ya mwenyekiti, Msigwa alisema mifumo ya chama imetumika kumhujumu asishinde na kumshutumu mwenykiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, kitendo alichosema kinaifanya Chadema kukosa uhalali wa kuikosoa CCM.
“Kama Chadema tunalalamikia Serikali ya CCM haitendi haki katika kusimamia uchaguzi, tulitakiwa tuwe mfano wa kuigwa lakini katika chaguzi zetu haki haitendeki.
“Hali hii inaleta mashaka na harufu ya uvundo wa ukiukwaji mkubwa wa haki ndani ya chama ambacho kinatakiwa kiwe mstari wa mbele katika demokrasia,” alisema Msigwa.
Hata jana akizungumza baada ya utambulisho huo, ofisi ndogo ya makao ya CCM, Lumumba, Msigwa alisema uamuzi wake wa kuhamia CCM umechochewa na hatua ya Chadema kukosa misingi na uhalali wa kukikosoa chama hicho tawala.
Katika mazingira hayo, amesema hakuona haja ya kuendelea kushindana, badala yake aungane na Serikali katika mambo inayoyafanya kama amani, utulivu na uhuru wa kuzungumza.
“Kwa kuwa tumepoteza misingi na tumekosa uhalali wa kuikosoa CCM, watu wenye akili, nimeona ni bora nishirikiane niungane na CCM,” alisema.
Machi mwaka 2020, alipohukumiwa kulipa faini au kwenda jela katika kesi iliyokuwa ikimkabili yeye na viongozi wengine saba wa Chadema waliolipa faini kwa kuchangiwa na wapenzi na wafuasi wa chama, yeye alilipiwa faini hiyo ya Sh38 milioni na Hayati Magufuli, kati ya Sh40 milioni zilizohitajika na kuibua mjadala, japokuwa ilielezwa kuwa Rais huyo alikuwa na uhusiano naye kifamilia.
Sambamba hilo, Msigwa alifuatwa na gari za Serikali na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM wa wakati huo, Humphrey Polepole, jambo ambalo liliongeza dhana za nasaba yake na chama tawala. Hata hivyo, Msigwa aligoma kupanda gari hilo, badala yake aliondoka kwa gari la wakili wa Chadema.
Lilikuwa suala la muda
Kutokana na matukio hayo na mengine, uamuzi huo wa kujiunga na CCM, umeeleza ulikuwa unasubiri tu muda, kama inavyoelezwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itifaki, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema.
Akizungumza na Mwananchi, Mrema alisema intelijensia ya Chadema ilishatoa taarifa za mwenendo wake na kulikuwa na dalili zote za Msigwa kujiunga na chama tawala.
“Tulikuwa tunasubiri muda ufike na muda umefika leo, kwa sababu ameamua kwenda CCM tunaendelea kukijenga chama chetu,” alisema.
Mrema amezihusisha harakati za Msigwa katika siku za mwisho mwisho ndani ya Chadema na vurugu za maandalizi ya kupandisha thamani yake ili aondokea.
“Hata uko CCM Mchungaji Msigwa akikosa cheo ataondoka,” alisema.
Kuhusu rufaa yake ya kupinga ushindi dhidi ya Joseph Mbilinyi “Sugu”, Mrema alisema ilikuwa isikilizwe katika kikao cha Baraza Kuu, kwa sababu mwanasiasa huyo alikuwa mjumbe wa kamati kuu.
“Tulikuwa tunasubiri chaguzi zote zimalizike ndipo tuitishe Baraza Kuu kujadili rufaa ya Msigwa, tusingeweza kujadili rufaa yake pekee, maana huenda zingine zingejitokeza na kufanya vikao mara kwa mara vya Baraza Kuu kwa kuwa ni gharama,” alisema Mrema na kuwa kwa uamuzi huo na mchakato wa kusikiliza rufaa yake utakuwa umejifia hapo.

Пікірлер: 5

  • @MajutoElliasi
    @MajutoElliasi2 күн бұрын

    Mpeni cheo cha mkuu wa mkoa ws wasatiti

  • @lutegoemilimmetishawazeewa3757
    @lutegoemilimmetishawazeewa37572 күн бұрын

    Njaa njaa njaa njaa njaa njaa mbaya sana

  • @dennisungonella205
    @dennisungonella2052 күн бұрын

    Haahaa fursa ndo kinachomtesa msigwa...Bila uongozi hawezi kuisha

  • @happymushi4493
    @happymushi44932 күн бұрын

    Upendo nae kama anataman ahojiwe

  • @fredrickmwakalinga6390
    @fredrickmwakalinga63902 күн бұрын

    Inamaana ccm bila kununua chadema hawana viongozi bora? Inamaana wana ccm ni mazombi

Келесі