FAHAMU ZAIDI KUHUSIANA NA MATUMIZI SAHIHI YA MIZANI

Malengo makubwa ya serikali kwenye uwekaji wa mizani katika barabara ni kudhibiti na kunusuru uharibifu wa miundobimu ya Barabara kote Nchini Ikumbukwe ya kuwa Serikali ya Awamu ya sita Kupitia Wakala ya Barabara Tanzania TANROADS imeendelea kuboresha, kutengeneza na kurejesha Miundombinu ya barabara na ujenzi wa viwanja vya ndege hapa Nchini.
Itakumbukwa kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) ikisimamiwa na Wizara ya Ujenzi imekamilisha ujenzi wa Mzani mpya wa kisasa wa Mikumi uliopo barabara kuu ya Morogoro - Iringa, pamoja na maboresho katika mizani ya mikese uelekeo wa barabara ya Dar-es Salaam - Morogoro kwa gharama ya shilingi bilioni 1.9, hatua ambayo imesaidia kumaliza msongamano wa magari katika barabara hizo. Na sasa mizani zote tatu za Mkoa wa MOROGORO hali ni shwari na ufanisi ni mkubwa.
Fuatilia makala hii ambayo imeandaliwa na kitengo cha habari na mawasiliano TANROADS baada ya kuweka kambi Mkoani Morogoro, Makala hii itatoa fursa ya kila mwananchi hususani maafisa usafirishaji (MADEREVA) kukufahamu kwa kina kuhusu matumizi sahihi ya Mzani.

Пікірлер

    Келесі