Wakazi wa Gesima, Nyamira, wanalalamikia huduma duni hospitalini

Baadhi ya wakazi wa eneo la Gesima, katika kaunti ya Nyamira wamelalamikia kudorora kwa huduma za afya na ukosefu wa dawa, katika hospitali ya kaunti ndogo ya Gesima.
Wakizungumza hospitalini humo, wakazi wamesema wanalazimika kutafuta dawa na huduma muhimu za afya katika hospitali za kibinafsi na duka za kuuza dawa, licha ya kuwa na hospitali ya daraja la nne katika eneo hilo.
Wenyeji wamesema baadhi ya huduma walizopata katika hospitali hiyo hapo awali kwa sasa hazipo, huku wakidai kwamba hakuna wahudumu wa afya kuwashughulikia
Waziri wa afya katika kaunti hiyo Donald Mogoi amedhibitisha baadhi ya malalamishi yaliyotolewa na wakazi hao, na kusema serikali ya kaunti ina mpango wa kutatua maswala hayo katika mwaka ujao wa kifedha.

Пікірлер