Jaji Warioba ataja mambo manne yazingatiwe Katiba Mpya

Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
Joto la mchakato wa Katiba mpya halijapoa baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba kusisitiza:
“Mjadala na mashauriano juu ya Katiba mpya unapaswa kuendelea hadi 2025.”
Jaji Warioba amebainisha maeneo makuu manne yanayopaswa kupata mwafaka wa kitaifa kabla ya kwenda kwenye kura ya maoni ya Katiba Pendekezwa ni suala la maadili, madaraka ya Rais, mambo ya uchaguzi na muundo wa Muungano.
Amesema mambo hayo yasipopata mwafaka itakuwa vigumu kwa Katiba Pendekezwa kuridhiwa na wananchi.

Пікірлер: 16

  • @ramamjema8391
    @ramamjema83913 ай бұрын

    Huyu Mh jaji mustafu namfuatilia sana ni zao la haki na mmoja wa watu wachache waadilifu na wenye misimamo kwa anachokiamini, taifa lingekuwa na utaratibu wa kuwatumia watu kama Hawa na kufanyia kazi mawazo Yao kwa dhati na hata kuwapa tuzo za heshima kwa kutumikia taifa kwa uadilifu, Mungu azidi kukubariki na akupe maisha marefu yenye baraka tele na amani.

  • @abdalahgunda1319

    @abdalahgunda1319

    3 ай бұрын

    When l following warioba advise to ccm leadership then ccm crush warioba advise is to show that this nation no darection of good leadership into ccm after ccm feel compation if political outcome use powerforce wich it has got no fiucher such leader mostly africa leadership when rool party feel to complite with opposition outcome use force at the end crush even peace remain a little into pablic sense wich sametime is the Denger in Africa leadership to have military police lteligince with powerful coruption people on leadership das not mine country can be manege rool national by airn face slightly mistake already put national on cares all this course by brutal election we still advise ccm leadership follow warioba advise to solve national not wasira or Abraham kinana this are not capacity of understand benefits of the nation are saif look rooling part not national benefits such people are pointless to advince rooling part are low capacity of saycology sense underground only look at part not national

  • @ibbyikh1788
    @ibbyikh17883 ай бұрын

    Kweli kabisa wabunge kuchaguliwa kuwa mawazili hiyo inaongeza ufisadi tuh, viwe vitu viwili tofauti.

  • @user-jj7qv7kh2s
    @user-jj7qv7kh2s3 ай бұрын

    Nakufuatilia sana mheshimiwa jaji, mstaafu.

  • @paull8659
    @paull86593 ай бұрын

    mzee wambie hao mafisi wa chama chako. wao wanataka kuunda nchi imwage damu ndiyo wakubali KATIBA MPYA.

  • @wakwetu2444
    @wakwetu24443 ай бұрын

    Ni kweli Jaji. Maadili hayapo.

  • @albertkamala6843
    @albertkamala68433 ай бұрын

    Shikamoo Mzee Warioba! Hakika ni miongoni mwa wazee wachache waliobaki waliojaaliwa busara na hekima na dhamira njema kulinusuri taifa kupambania mabadiliko chanya ya taifa. Mahakama na Bunge ni mihimili inayopaswa kuwa huru!

  • @MrA24G
    @MrA24G3 ай бұрын

    Kikatiba iwe katiba ambayo kila mhimili una kazi yke.

  • @namsifubwana2152
    @namsifubwana21523 ай бұрын

    MUNGU AKUBARIKI SANA JAJI WARIOBA

  • @adelinelyaruu3036

    @adelinelyaruu3036

    2 ай бұрын

    Tuna Imani na wewe Mheshimiwa Warioba. Pigania kile unachokiamini ili tupate KATIBA MPYA. We were almost there

  • @DevothaLighton-dl6zi
    @DevothaLighton-dl6zi3 ай бұрын

    Ni kweli mzee,hawa wanataka kumwaga damu kwanza na nina hakika hii katiba italeta machafuko.kweli mpakawa leo fisiem wanatuchagulia watu kweli?

  • @SalehRashid-zz7dc
    @SalehRashid-zz7dc2 ай бұрын

    wazanzibari waulizwe wanautaka au hawautaki? 😊

  • @DevothaLighton-dl6zi
    @DevothaLighton-dl6zi3 ай бұрын

    Hili jambo la katiba natume huru italeya machafuko,shime fisi em.msikilize huyo mzee.kwa sasa hata mkifanya zuri ni baya tu mpaka katiba mpya

  • @dismasmtui729
    @dismasmtui7293 ай бұрын

    Mawaziri kutokuwa Wabunge ingepunguza kujipendekeza na uchawa

  • @BonaventureJohn-mk6xh
    @BonaventureJohn-mk6xh2 ай бұрын

    Chaguzi zetu za sasa zisipofanyiwa marekebisho serious itakuwa kutukaghai wananchi na ni kuchezea Kodi zetu maana ni muujiza mechi ya Simba na yanga refa awe Mo, washika kibendera wawe Mangungu na Try Again halafu utegemee yanga apate haki

  • @hajihassan5433
    @hajihassan54332 ай бұрын

    Mzee Warioba tume yako ililazimisha uwepo wa Muungano. Ungeacha mawazo huru tukaona Watanzania bado wanauhitaji Muungano au la. Shida yote iliyopo ni kwamba Wazanzibar na Watanganyika wote wamechoka na Muungano na ndio msingi wa Katiba ilipo. Ni dhahiri Watanganyika ambao ndio wamevaa utanzania wamesahau uwepo wa Zanzibar ambayo ni mshirika wa Tanzania kwa 50%. Matokeo yake Katiba HAIHESHIMIWI wala HAITEKELEZWI hivyo hata Katiba Mpya ni kazi bure. Maadili ni mtu mwenyewe. Rais Magufuli alirekebisha maadili na heshima kwa Watumishi kwa Katiba hii hii.