Wakulima wa kahawa wapewa miche Kericho

Wakulima wa kahawa wametakiwa kutia maanani katika kilimo hicho ili wafaidike na mazao hayo.
Akizungumza baada ya kutoa miche ya kahawa kwa zaidi ya wakulima mia tano kutoka Momoniat eneo bunge la Kipkelion, mbunge Joseph Cherorot amesema kilimo cha kahawa kina manufaa kwa wakaazi hao na ipo haja ya kila mkulima kutunza mimea yake ili kupata mazao bora. Aidha kuna mipango ya kushirikiana na wazee wa kijiji ili kuhakikisha kwamba kila mkulima aliyepata miche ya kahawa ataweza kupanda na kuitunza kwa njia inayofaa.

Пікірлер

    Келесі