Wakaazi wa magharibi wametakiwa kujibidiisha kazini

Wakaazi wa eneo Pana la magharibi wametakiwa kubuni mbinu mwafaka za kujiimarisha kimaisha badala ya kutegemea msaada kutoka Kwa wahisani na serikali.
Akizungumza baada ya kongamano la muungano wa makanisa ncck tawi la magharibi ,naibu gavana wa kaunti ya Bungoma jenipher mbatiany amesema eneo hilo linasalia nyuma kimaendeleo kutokana na hulka ya watu wanaopenda kusubiri msaada. Amewataka vijana kujitwika jukumu la kuwekeza Katika Kilimo biashara badala ya kutegemea kuajiriwa.
Aidha kasisi wa kanisa la ACK Bungoma George mechumo amewataka wabunge kuupiga msasa mswada wa fedha unaotarajiwa kujadiliwa bungeni Na kufanya maamuzi ya hekima Kwa niaba ya wananchi ili kuimarisha maisha ya wakenya.

Пікірлер