Rais wa Rwanda Paul Kagame anaelezea kwanini Afrika ni MASIKINI.

Rais wa Rwanda Paul Kagame anaelezea kwanini Afrika ni MASIKINI.
Wakati akihojiwa na Aljazeera siku kadhaa zilizopita Rais Kagame alisema kuwa suala la unyonyaji wa nchi za Afrika hufanywa na mataifa yote makubwa.
Mwandishi alimuuliza "Je, Wafaransa, Wamerekani, Wabelgiji na Wachina wanahusika katika unyonyaji wa Afrika?". "Ndio wote wahausika" Kagame alijibu.
Pia alisema "Afrika ni tajiri mno katika maliasili na rasilimali watu, sidhani kama kuna sehemu nyingine ya duniani imebarikiwa vitu vya namna hiyo kama Afrika.. Lakini changamoto inayokuja niyakiutawala namna ambavyo hizo nchi zinajitawala zenyewe na namna ambavyo serikali zinashirikisha watu wake kwenye kila kitu inachofanya".
"Kwa mfano hizi nchi ambazo zimekwisha endelea ambazo sasa zipo Kila nchi ya bara la Afrika wanakuja, kuwafundisha Waafrika demokrasia, haki za binadamu na uhuru alafu mwisho wa siku wananyonya maliasili zetu na kujitengenezea pesa kupitia makampuni Yao na wakati mwingine nchi hizo zinajihusisha moja kwa moja katika unyonyaji huo" Kagame aliongeza.
Kwa maelezo hayo ya Mhe Paul Kagame inaeleza kuwa hakuna nchi mbadala wa kuisaidia Afrika bila Afrika kujisaidia yenyewe haijilishi ni China au Ufaransa. "AFRIKA LAZIMA IJIFUNZE KUJILISHA MWENYEWE".
Nini mtazamo wako kuhusu maoni ya Mhe. Paul Kagame?.
#AFRICAISOURS

Пікірлер

    Келесі