MILIONI 400 KUKOMESHA MAFURIKO IFAKARA.

Serikali imetoa zaidi ya shilingi Milioni 400 kujenga tuta kubwa kuimarisha kingo za Mto Lumemo uliokatiza kwenye Mji wa Ifakara, kuepusha madhara yanayo jitokeza zinaponyesha mvua kubwa, msimu wa mwaka huu pekee kuna zaidi ya watu 10 waliopoteza maisha kwa kusombwa na Maji
Mradi huo mkubwa unalenga kurejesha maji yaliyokuwa yakipotea kipindi cha Mvua, kwa kutapakaa baada ya Mto kupoteza uelekeo, tayari ujenzi wa tuta kubwa umekwisha anza kuna zaidi ya asilimia 45 zilizofikiwa, takribani kilomita 4 kati ya 12 zilizopangwa kama inavyo elezwa na Msimamizi wa Mradi afisa Maji Bonde la Rufiji Kidakio cha Kilombero.
Mto Lumemo ni kati ya Mito mikubwa unaochangia asilimia 35 ya Maji yaliyo kwenye Mto Kilombero ambao ndio unaojaza Bwawa la Mwalimu Nyerere kwa zaidi ya silimia 65, mradi huo pamoja na kulenga kutafutia suluhu mafuriko kwenye mji wa Ifakara utasaidia pia uendelevu kwenye wa Maji kwenye bwawa la Nyerere.

Пікірлер

    Келесі